Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na siyo kumtishia mbunge huyo.
Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza sana Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa series ya matukio hayo yanayohusisha rushwa.
Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.
"TAKUKURU siyo mahakama na kwa kweli haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro
Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?
Pamoja na hayo Mtatiro amesema kutokana na kauli za Mkurugenzi wa TAKUKURU haitabaki salama kwa kauli na mienendo ya namna hiyo ikiendelea kutolewa.
Tuesday, 17 October 2017
Home
Unlabelled
Mtatiro amjia juu Mkurugenzi wa Takukuru kuhusu ushaidi wa Nassari
Mtatiro amjia juu Mkurugenzi wa Takukuru kuhusu ushaidi wa Nassari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment