Mbunge wa Tarime John Heche ameikosoa serikali ya Rais Magufuli - KULUNZI FIKRA

Thursday, 26 October 2017

Mbunge wa Tarime John Heche ameikosoa serikali ya Rais Magufuli

 
Mbunge wa Tarime  Vijiji, John Heche amekosoa uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba na kusema kwamba fedha zinazotumika katika kufanya uchaguzi huo zingesaidia katika kuwapatia mikopo wanafunzi.

Mbunge John  Heche amelazimika kukosoa uchaguzi huo ambao Tume ya Uchaguzi imetangaza kwamba utafanyika mwezi Nov 26 katika Kata 43 huku kukiwa na madai ya kwamba kuna baadhi ya Madiwani walikuwa wamenunuliwa ili kuvihama vyama vyao.
Ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba.  

"Mmetumia pesa kununua madiwani sasa mnatumia pesa za umma kufanya uchaguzi, pesa hizo zingetumika kuwapa mikopo wanafunzi wanaoteseka" alisema John Heche.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba,  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuwa kutakuwepo kwa uchaguzi wa marudi mwezi Novemba  katika kata 43 ambazo madiwani wake walijiuzulu, wengine wakiwa wamefariki huku wengine wakiwa wametenguliwa na mahakama kwa kushindwa kuhudhuria vikao.

No comments:

Post a Comment

Popular