Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa Mjini na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.
Peter Msigwa amesema hayo jana jijini Dar es salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
"Iringa Mjini biashara nayo ilifanyika. Nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Polisi, hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri.
"Kwa hivyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za Serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa Serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua". alisema Mchungaji Peter Msigwa.
Monday, 2 October 2017
Home
Unlabelled
Mbunge Peter Msigwa awataja waliohusika kununua madiwani Iringa
Mbunge Peter Msigwa awataja waliohusika kununua madiwani Iringa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment