Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshinda pingamizi dhidi ya Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini na watu wake katika kesi ya bodi ya Udhamini - RITA
Leo Oktoba 5, 2017 katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera imetoa maamuzi juu ya mapingamizi yaliyowekwa na Lipumba aliyekuwa akiwakilisha na Wakili Mashaka Ngole na Majura Magafu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Shauri (Namba Miscilleneous Civil Application No. 51/2017) kuhusu CUF kuomba kuwazuia Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa na Lipumba wasifanye kazi ya Bodi hiyo mpaka pale shauri la msingi Namba 13/2017 litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu.
Jaji Wilfred ameyatupilia mbali mapingamizi hayo kutokana na kutokuwa na hoja za msingi za kisheria. Mhe Jaji amekubaliana na hoja zilizowasilishwa na Mawakili upande wa CUF unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho akiwepo Mhe Fatma Karume, na Mhe. Mpoki Kabe.
Kufuatia maamuzi hayo yanatoa nafasi ya kwenda kusikilizwa kwa undani wa hoja zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Ally Salehe ambaye ndiye muombaji
Hoja za pande zote mbili zitawasilishwa kwa maandishi kwa utaratibu mpaka Oktoba 19, 2017 Ally Salehe ambaye ni muombaji anapaswa kuwa amewasilisha huku Oktoba 17, 2017 upande wa walalamikiwa wanapaswa kuwa wawe wamejibu na mnamo Novemba 6, 2017 Ally Salehe awasilishe majibu zaidi na tarehe 7, Novemba kesi itatajwa kwa kupagwa siku ya kutolewa Maamuzi.
Thursday, 5 October 2017
Home
Unlabelled
Mahakama yatupilia mbali shauri la pingamizi la Prof Lipumba dhidi ya Cuf
Mahakama yatupilia mbali shauri la pingamizi la Prof Lipumba dhidi ya Cuf
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment