Lowasa alaumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa chama cha mapinduzi (CCM) - KULUNZI FIKRA

Sunday, 8 October 2017

Lowasa alaumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa chama cha mapinduzi (CCM)

 Mzee mtulivu Edward Lowasa amelaumia na viongozi wa juu wa CCM kwamba anaingilia chaguzi zinazoendelea CCM.

Lowasa ambaye alishahama chama hicho toka 2015 amekuwa akilaumiwa kutokana na kuendelea kutajwa kwa kutolewa mfano na wanachama wa CCM.

Baadhi ya wanachama wa CCM wametishiwa kutimuliwa chamani kutokana na kuendekeza mapenzi yao kwa Lowasa.

Kauli ya Lowasa aliyotoa jana na kushika kasi juzi na Jana  ikiripotiwa katika magazeti,imekichanganya chama na kuzidisha lawama. Lowasa amenukuliwa akiwataka wana CCM wanaovutiwa na demokrasia wahamie Chadema na UKAWA kufaidi matunda ya nchi yao.

Lowasa amesisitiza kuwa hata wale watakao bakia CCM wamuunge mkono wakiwa hukohuko kwani chama chao kinawakatisha tamaa

No comments:

Post a Comment

Popular