Halima Mdee: Wanawake ndio chachu ya Ushindi uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 - KULUNZI FIKRA

Sunday, 22 October 2017

Halima Mdee: Wanawake ndio chachu ya Ushindi uchaguzi mkuu wa mwaka 2020


Mwenyekiti wa Baraza la wanawake la chadema Taifa ( Bawacha) Mhe Halima Mdee amesema wanawake wakiwezeshwa na kupewa mafunzo ya kujitambua watakuwa chachu ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na wanawake wa jimbo la Segerea jijini Dar es salaam leo jumapili oktoba 22, 2017 amesema wamekuwa wakitumika kama daraja pasipo wao kujijua. Mhe Halima Mdee amesema kutokana na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume,wakiamua kufanya mageuzi wanaweza ila wanahitaji kujengewa ujasiri.

"Wanawake wakijitambua na hasa wakipatiwa mafunzo ya ujasiri wataweza kuwa mkombozi wa jamii na Taifa kwa ujumla katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020," amesema Mhe Halima Mdee.

Mhe Halima Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, amesema kupitia semina hiyo wanawake hao watajua nafasi zao katika jamii na kuwa na uwezi wa kufanya uamuzi wowote wenye tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.

"Tunaona matukio ya ajabu yanatokea watu wanatekwa , kamanda wetu Tundu Lissu alishambuliwa kwa kupigwa risasi na ameweza kupata nafuu tujue Mungu ana makusudio yake,hivyo nasi wanawake tujue cha kufanya katika Taifa hili," amesema mwenyekiti wa Bawacha wa jimbo la Segerea , Agnester Lambati amesema," Tumeamua kumuita Mhe Halima Mdee aje kuongea na sisi wanawake wa Segerea tukitambua mchango wake wa kuwapigania wanawake wa nchi hii usiku na mchana".

Awali, Mhe Halima Mdee alifungua ofisi ya Bawacha ya jimbo la Segerea pia alimkabidhi kadi ya uanachama Florence Makongoro ambaye ni mke wa mwenyekiti wa chadema jimbo la Ilala , Dkt Makongoro Mahanga.

No comments:

Post a Comment

Popular