Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha wanasheria Tundu Lissu, imemshauri Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro kuchukua hatua za kumfuata dereva wa Lissu, Jijini Nairobi na siyo kumuita aje kwa ajili ya Mahojiano
Wakizungumza Jana na wanahabari, Kaka wa Tundu Lissu ambaye pia ni Wakili, Alute Mughwai Lissu amesema kwamba, Jeshi la polisi kama wameona kwamba dereva wa Lissu anaweza kuwa msaada kwa ajili ya upelelezi wao basi watumie ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kufanya naye mahojiano na dereva huyo.
Mughwai amesema kwamba kitendo cha kukaa kwa takribani mwezi mzima kwa ajili ya kumsubiri Dereva wa Lissu wangekuwa wameshakwenda Nairobi na wakawa wameshapata maelezo wanayohitaji.
"Siku zote dereva yupo hospitalini anamuuguza bosi wake. Wakamchukue pale waende nao kwenye ofisi za Ubalozi na wachukue maelezo badala ya kusubiri. Katika tukio la shambulio la Lissu kama dereva angekufa inamaana wangeacha upelelezi si wangeeendelea? Basi wafanye upelelezi kwa njia hiyo na siyo kumuita arudi nchini ili kumhoji". amesema Mughwai
Mughwai amehoji kwamba "Mpaka sasa kama watu hawajakamatwa, je wanamuhakikishiaje usalama dereva huyo, isije akatoka huko kuja kuhojiwa alafu akiwa anapita Namanga anakuja anakatishwa usalama wake njiani. Na kama wataenda kumchukua busara inaeleza kwamba aweze kuhifadhiwa ahakakikishiwe usalama wake, achukuliwe maelezo na ahifadhiwe siyo jela kwani yule ni shahidi tu.
Ameongeza kwamba wao kama famillia hawana maslahi na chama chochote na hawako tayari kuona jambo la shambulio la ndugu yao likafanywa siasa bali wanachotaka ni shambulio hilo liweze kufanyiwa uchunguzi pamoja na ndugu yao kupona.
Hata hivyo mdogo wa Tundu Lissu Vicenti Mugwai amewashukuru Watanzania wanaofanya maombi kwa Lissu pamoja kuendelea kuwatolea michango kwa ajili ya matibabu ya ndugu yao
Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya 30 katika gari lake na zaidi ya tano inadaiwa kumpata mwilini mwake mnamo Septemba 7 , 2017 majira ya mchana nje ya makazi yake Area D Dodoma.
Thursday, 5 October 2017
Home
Unlabelled
Familia ya Tundu Lissu yatoa mbinu za kumkamata dereva wa Lissu
Familia ya Tundu Lissu yatoa mbinu za kumkamata dereva wa Lissu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment