Ester Bulaya amjia juu Mwigulu Nchemba kuhusu watu wasiojulikana - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 4 October 2017

Ester Bulaya amjia juu Mwigulu Nchemba kuhusu watu wasiojulikana

 Mbunge wa Bunda Mjini Kupitia CHADEMA, Ester Amos Bulaya, amemtaka Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, kuwataja watu wanaofanya uhalifu ikiwepo kuwatishia maisha baadhi ya viongozi hapa nchini ikiwepo Nape Nnauye kwani anawajua.

Bulaya ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa kulunzifikra blog na kusema kwamba Waziri anawajua watu hao lakini anaogopa kuwataja kwa kulinda kitumbua chake kuingia mchanga.

Ester Bulaya ameendelea kusema kwamba kitendo hicho sio kizuri kwani kinaweza kutokea kwa watu wengine ikiwemo familia yake, na hivyo atashindwa kuchukua hatua kama ambavyo anafanya sasa.

No comments:

Post a Comment

Popular