Dar es salaam: Kamanda Mambosasa alaani kitendo cha wananchi kushambuliwa na askari maeneo ya ukonga - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 24 October 2017

Dar es salaam: Kamanda Mambosasa alaani kitendo cha wananchi kushambuliwa na askari maeneo ya ukonga

 Ndugu zangu wanahabari nimewaita mchana huu ili niweze kutoa taarifa moja tu inayohusiana na kanda maalum ya Dar es salaam  kulaani vikali maauwaji ya Askari wa Polisi wa kikosi cha kuliza ghasia makao makuu ya jeshi pale Ukonga

Lakini pia Jeshi la Polisi linalaani vikali vitendo vya kihuni vya wananchi kushambuliwa katika maeneo hayo ya Ukonga

Mnamo tarehe 21/10/2017 Jeshi la Polisi kanda maaalum ya Dar es salaam  kwenye majira ya saa sita usiku huko maeneo ya kambi ya jeshi la Polisi. Kikosi cha kutuliza ghasi Ukonga makao makuu alfajiri mwili wa askari Polisi mwenye namba XG475PC Charles Yanga uliokotwa uliolkotwa pembeni au kando ya uzio wa kambi hiyo huko Ukonga ukiwa umeangushwa chini huku pikipiki yake ikiendelea kuwaka zile taa za 'Hazard'

Mwili ulipochunguzwa majeraha yalionekana kwenye paji la uso la kijana huyo ambaye alikuwa teyari amesha fariki dunia lakini pia sikio moja lilikuwa limekatwa na kuondolewa kabisa

Katika Ufuatiliaje wa polisi walibaini kuwa askari huyo aliuwawa na watu ambao bado wanafuatiliwa na hatujafanikiwa kuwatia mbaroni bado. polisi kupitia kikosi kazi chake kinaendelea na kazi yake ya upelelezi kufuatila watu walitenda mauwaji ya polisi wetu Charles Yanga. wakikamatwa hatua zitachukuliwa ikiwa ni pamboja na kuwapeleka mahakamani

Wakati huohuo;
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam  manamo 22/10/2017 lilipokea malalamiko la watu wanaosemekana ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia Ukonga kuendelea kushambulia wananchi maeneo ya Ukonga, Mazizini na maeneo mbalimbali ya eneo hilo

Wananchi waliotoa taarifa ni kwamba akuna watu wanasambaa usiku wakiwa wanawakamata wananchi, kuwapiga, kuwadhalilisha akina mama, na wengine pia wametoa taarifa za kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Popular