Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula, zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea wiki iliyopita katika maeneo ya Kurasini na kwamba, mtuhumiwa alitiwa mbaroni baada ya wasamaria wema kuripoti kitendo hicho.
“Tukio hili lina muda… nadhani wiki imepita sasa kwa sababu tunalifanyia uchunguzi wa kina. Sikutaka kulizungumza, ila ni kweli tukio lipo na hayo mengine tunaendelea na upelelezi wetu," alisema Kamanda Lukula kuelezea tukio hilo.
Awali, vyanzo vya habari viliambia kulunzifikra blog kuwa askari huyo alimbaka mtoto wa chekechea katika ambayo alionekana akiwa amelewa chakari.
“Hiyo siku ya tukio, huyo askari inadaiwa alikuwa kalewa sana… nimeshindwa kumwelewa. Hizo ni pombe gani hadi ambake mtoto wa miaka sita wakati wanawake wako wengi,” alisema mtoa taarifa, huku akidai kuwa mtuhumiwa huyo ni askari katika kituo kikuu cha polisi na amewashangaza wengi kwa tukio hilo nadra kuwahusisha polisi ambao ndiyo wenye jukumu la kuwalinda raia na mali zao na pia kusimamia sheria za nchi.
Chanzo kilieleza zaidi kuwa mtoto aliyefanyiwa unyama huo alichukuliwa vipimo kwenye hospitali inayotambulika na mwishowe madaktari walibaini kuwa ni kweli alibakwa.
Chanzo kiliambia zaidi kulunzifikra blog kuwa askari anayetuhumiwa kwa ubakaji ni mpangaji kwenye nyumba ya uraiani ambayo mtoto aliyebakwa anaishi na bibi yake.
Akielezea zaidi kuhusu hatima ya mtuhumiwa, Kamanda Lukula alisema bado yuko mahabusu na uchunguzi zaidi dhidi yake unaendelea kabla ya kufuatiwa na hatua za kisheria.

No comments:
Post a Comment