Chadema imesema haitashiriki uchaguzi wa naibu meya unaotarajiwa kufanyika katika Manispaa ya Kinondoni.
Katibu Mkuu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo leo Jumanne Oktoba 31,2017 ameieleza kulunzifikra blog kuwa, baada ya kikao cha madiwani wa mkoa na baadhi ya viongozi wamekubaliana kutoshiriki uchaguzi huo.
Uchaguzi wa naibu meya hufanyika kila mwaka nchini ikiwa ni utekelezaji wa sheria.
"Hatutashiriki kwa sababu tulifungua kesi Mahakama Kuu inayopinga uhalali wa Meya wa Kinondoni, kwa hiyo kushiriki itakuwa ni kuhalalisha tunachokikataa mahakamani," amesema.
Kilewo amesema wiki iliyopita ofisi yake ilipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli ikitaka kupendekeza jina la mgombea wa nafasi hiyo kabla ya Oktoba 30,2017.
Akizungumzia kauli ya Chadema, Kagurumjuli amesema hakuna barua aliyoipata kuhusu uamuzi huo.
Amesema ofisi yake imepokea jina la mgombea wa CCM leo Jumanne Oktoba 31,2017 na inasubiri vyama vingine vya CUF na Chadema.
"Sina taarifa ya maandishi ya chama chochote kususia uchaguzi. Hata kama wasipoleta jina hawataathiri uchaguzi, wakikaa kimya maana yake hawana mgombea, sisi tutaendelea na uchaguzi na utaratibu ukikamilika uchaguzi utafanyika," amesema.
Katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 23,2016 Benjamin Sitta alichaguliwa kuwa meya, huku George Manyanya akichaguliwa kuwa naibu meya.

No comments:
Post a Comment