Mbunge wa Tarime Vijijini , John Heche amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro kutangaza kiama kwa wahalifu wa wanaofanya mauaji kwa kupiga watu risasi siyo na siyo kuwatangazia wakosoaji wa Serikali.
Heche amelazimika kusema hayo baada ya hivi karibuni IGP Sirro alipokuwa mkoani Iringa kusema kwamba anafahamu makosa ya mtandaoni yanayofanywa na Mange Kimambi na kuahidi kwamba watamshughulikia.
"IGP anapaswa kuwatangazia kiama wahalifu na watu wanaofanya vitendo vya kupiga watu risasi na kutupa wengine baharini sio wakosoaji wa serikali"
Aidha Kiongozi mwingine wa Chadema aliyeingilia kauli ya IGP Sirro kuhusu Mange Kimambi ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye yeye alsema,
"IGPSirro shughulika na usalama wa raia, malizia uchunguzi BenSanane, TunduLissu na maiti zinazookotwa baharini. Achana na Mange Kimambi"
Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro alisema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mtanzania Mange Kimambi aishiye nchini Marekani na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia suala hilo.
Thursday, 12 October 2017
Home
Unlabelled
Chadema wamjia juu IGP Sirro kuhusu kumtafuta Mange Kimambi
Chadema wamjia juu IGP Sirro kuhusu kumtafuta Mange Kimambi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment