Ayoub Rioba : Ukusoaji halijawahi kuwa jambo baya katika Taifa - KULUNZI FIKRA

Sunday, 29 October 2017

Ayoub Rioba : Ukusoaji halijawahi kuwa jambo baya katika Taifa

 
 Akiwa kwenye mfululizo wa vipindi vinavyoangazia miaka miwili ya utawala wa awamu ya tano ambapo leo waliongelea mchango wa vyombo vya habari katika ujenzi wa Tanzania, mkurugenzi wa TBC, Dokta Ayoub Rioba amesema tunapokwenda inawezekana vijana wengi wasijue uzito, ugumu na madhila kuishi kama walivyoishi na kunyonywa kama walivyonyonywa.

Amesema mambo kama yaliyotokea juzi, Barrick kuja kukaa meza moja na Tanzania na kuzungumza mpaka walipofikia watu wasidhani kuwa ni tukio dogo rahisi, hayatokei na watu wafanye utafiti, amesema watu waulize nchi nyingine hali ikoje ukiacha nchi chache kama Botswana na Afrika kusini. Amesema hasa vijana waelewe hili si jambo dogo kwani kinachofanyika sasa ni kwa niaba yao na nchi yao ili isije kufika mahali nchi ambayo ina mali nyingi watu wake wanaendelea kuwa masikini, kunakuwa na viwanja vya ndege na watu wanakuja kuchukua mali na sisi tumekaa kama mazuzu na chupa tukisema ndio almasi tumeachiwa(Mwanzo alitolea mfano).

Rioba amesema kwa mtazamo wake, vyombo vingi vya habari vimefanya kazi nzuri na viendelee kufanya kazi nzuri hasa ya kuwaunganisha watanzania lakini pia viwe tayari kukosoa pale ambapo vinaona kuna mambo yanafanyika lakini hayasaidii mwelekeo ambao wangependa kwenda kwani ni kazi muhimu sana ya vyombo vya habari.

Rioba amesema nchi hii ni yetu sote na amesema wakati wao wa JKT hawakuwa na chuki na ubaguzi ambao umeenea sana katika miaka ya karibuni. Ametolea mfano wa professa wa kinaijeria ambae alisema wao wanaijeria wako vizuri sana katika kujikosoa lakini wakati mwingine tunapeleka kujikosoa mbali mno katika kiwango cha kujiumiza wenyewe.

Rioba amesema kukosoa ni jambo zuri na halijawahi kuwa jambo baya lakini kuna namna ambayo tunavyojiandika wenyewe, tunavyojisema na kusemana wenyewe itaishia kutuumiza kama jamii tena katika wakati ambao tulitakiwa kuja pamoja. Amesema ni Rai yake vyombo vya habari vije pamoja na kusaidia watanzania kuona kwamba tuna tofauti zetu lakini hazisababishi tuwe maadui na tutaendelea kuishi katika taifa moja.

No comments:

Post a Comment

Popular