Spika wa Bunge, Job Ndugai amewatadharisha wabunge kuwa makini na usalama wao mahali popote wanapokwenda kufuatia matukio mengi ya uhalifu nchini.
Akizungumza muda mfupi leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai aliwataka wabunge kutokaa sana katika mabaa.
“Yaani tuchukue hatua tu katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe kwanza,”amesema.
Amesema vyombo vya usalama vinavyowalinda vinakuwa vinaongezea kidogo na kuwataka kutazama nyendo zao za namna ambavyo wanaishi.
“Kwa wale tuliozoea sana saa 7 ndio tunarudi nyumbani basi tuanze kurudi mapema kidogo. Lakini pia tuangalie usalama wa familia zetu na tuwaambie wapigakura naona siku hizi watoto wanapotea, watoto wanauawa,”amesema.
Amewataka wabunge kuwapelekea huo ujumbe kuwa wawe makini na watoto wao wakati wa kwenda shule na maeneo mengine kwa kuhakikisha wanajua mtu anayewapeleka shule na kuwachukua.
“Hayo mambo yanayofanana na hayo. Ushauri ni wa ujumla tu,”amesema.
Aliwataka wabunge kuendelea kumuombea Tundu Lissu na wale watakaopata nafasi ya kwenda kumuona jijini Nairobi wampelekee ujumbe.
Amesema pia wabunge wawaombee wenzao ambao wamekwenda kumuuguza mbunge huyo lakini wanatukana kwa sababu hawajui watendalo.
Ushauri huo umekuja siku chache baada ya Lissu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Friday, 15 September 2017
Home
Unlabelled
Spika awatahatharisha wabunge kuhusu usalama wao
Spika awatahatharisha wabunge kuhusu usalama wao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment