Rais Magufuli: Najuta kuwa Rais - KULUNZI FIKRA

Saturday, 23 September 2017

Rais Magufuli: Najuta kuwa Rais

 Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema anajuta kuwa rais kutokana dosari nyingi alizozikuta karibu kila sehemu ikiwemo ufisadi na wafanyakazi hewa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wakazi wa Arusha waliohudhuiria kushuhudia zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa JWTZ 422 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.

Amesema “Nimeamua kuwa sadaka kwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi... naamini hapatatokea mwingine atakayejitoa hivi”

Kuhusu Kuhamia Dodoma, amesema mwaka huu makamu wa rais atahamia Dodoma na mwakani yeye mwenyewe atahamia huko huku akionya watakaobaki Dar es Salaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Katika hatua rais Magufuli ametangaza ajira mpya 3,000 za jeshi ili kuongeza nguvu kazi katika jeshi la wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Popular