Omog awashiwa taa nyekundu ndani ya klabu ya Simba SC - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 13 September 2017

Omog awashiwa taa nyekundu ndani ya klabu ya Simba SC

Kunafukuta! Ndivyo ilivyo, kwani baada ya klabu ya Simba SC kupata safe bila kufungana dhidi ya klabu ya Azam FC wiki iliyopita huku ukiwa na wachezaji kibao wa wenye kiwango cha juu, kocha mkuu wa wa timu ya Simba SC, Mcameroon Joseph Omog amepewa mechi tano za kutathmini ajira yake ndani ya klabu ya Simba SC.

Taarifa zilizopatikana Jana jioni Dar es salaam zinaelezea kuwa uongozi wa klabu ya Simba SC umeonyesha kutoridhishwa na upangaji wa timu unaofanywa na Joseph Omog, na kudai ndiyo moja ya sababu ya timu yao kushindwa kupata idadi nzuri ya magoli katika mechi mbalimbali walizocheza kuanzia kipindi cha maandalizi ya msimu huu.

Akizungumza na kulunzifikra blog mmoja wa viongozi wa juu wa timu hiyo, alisema baada ya kufanikiwa kusajili wachezaji wenye uwezi katika idara zote wanatarajia kuona Simba SC 'haitaabiki ' kusaka ushindi, Lawama zote wameziamishia kwa kocha.

Kiongozi huyo alisema mbali na kushindwa kupata magoli mengi, pia kocha huyo analalamikiwa kwa kuchelewa kufanya mabadiliko wakati mechi inaendelea licha ya baadhi ya wachezaji kuonyesha kuwa mechi imewakataa na kusababisha mashambulizi kupungua.

" Ni kweli hilo jambo, ameelezwa na amepewa mechi tano na kuanzia ya Mwadui FC ambayo itachezwa jumapili, Simba ya sasa haipaswi kushindwa" alisema kiongozi huyo.

Kocha msaidizi w wekundu hao wa msimbazi,Jackson Mayanja aliambia kulunzifikra blog kuwa kikosi chao kinaendelea vizuri na mazoezi na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi  mnono dhidi ya Mwadui FC itakayopigwa uwanja wa Uhuru.

Tunajua huko mbele mambo yanaweza kuwa magumu zaidi na hasa kilichotokea msimu uliopita wote mnajua, tunataka kuona kila mechi tunashinda zaidi ya magoli matatu",  alisema Mayanja.

Baada ya mechi hiyo dhidi ya Mwadui FC, mabingwa hao wa kombe la FA, watasafiri  kuelekea Mwanza kuwafuata Mbao FC katika mechi nyingine ya ligi kuu Tanzania bars itakayofanyika septemba 21 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment

Popular