Nairobi: Bunge lamnyang'anya Freeman Mbowe gari la kiongozi wa upinzani Bungeni alilokuwa akilitumia - KULUNZI FIKRA

Thursday, 28 September 2017

Nairobi: Bunge lamnyang'anya Freeman Mbowe gari la kiongozi wa upinzani Bungeni alilokuwa akilitumia

Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe amenyang'anywa gari.

Taarifa kutoka Nairobi zinasema Bunge limeamuru kumnyang'anya mara moja gari kiongozi huyo bila taarifa zozote za ziada.

Watu kadhaa wamelaani uamuzi huo wa bunge chini ya Spika Ndugai na kusema hiyo ni chuki kubwa dhidi ya Upinzani Tanzania na dhidi ya Mbunge Tundu Lissu aliyepigwa Risasi na kunusurika kuuawa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumika kwa shughuli za matibabu ya Tundu Lissu jijini Nairobi .

Chadema imesema Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, aliamuru gari hilo lipelekwe Nairobi kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa chama hicho

Lissu ambaye pia Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na yuko Nairobi kwa matibabu.

Mkuu wa Idara ya Uenezi Chadema, Hemed Ali ameeleza hayo leo Alhamisi wakati akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu na kwamba hawana wasiwasi na hatua hiyo kwa kuwa wana marafiki wengi wakiwamo Watanzania waishio nchini humo na Wakenya wenyewe ambao kwa namna moja au nyingine watashirikiana nao.

Akizungumzia suala hilo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amedai kuwa hana na taarifa hizo, ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwa mwandishi na alimtaka mwandishi amuulize huyo aliyetoa taarifa kama kweli ametumwa na Mbowe.

“Naomba uumulize aliyesema taarifa hizi je ametumwa na Mbowe? Kwa sababu napata shida Mbowe ni kiongozi pale bungeni na ana wasaidizi wake na haya mambo ni ya ndani ndiyo maana nataka kujua huyu aliyetoa taarifa amezungumza kama nani? Alihoji Dk Kashililah.

“Haya mambo yana taratibu zake za kiofisi naomba niishie hapa. Maana tukiendelea nitakuuliza maswali ambayo utashindwa kuyajibu. Pia na utatakakujua mengi ikiwamo hata posho ya dereva wa Mbowe,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Popular