Mamia ya wananchi, viongozi wa CCM na matajiri wakubwa wa mji wa Geita wamemiminika katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi Geita wakisubiri kupandishwa mahakamani kwa Mbunge wa Geita Vijijini, Joesph Msukuma na madiwani kumi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa kusababisha vurugu zilizotokea Septemba 14 mwaka huu.
Walianza kufika mahakamani majira ya saa nane mchana wa Jana Jumatatu baada ya taarifa kuanza kuenea kuwa watapandishwa mahakamani lakini hadi kufika majira ya saa 9:20 alasiri Katibu wa CCM Mkoa wa Geita, Adam Ngalawa akatangaza kuwa viongozi hao hawatafikishwa tena mahakamani kutokana na muda wa Mahakama kumalizika.
“Tulikua tunawasubiri wenzetu tuwawekee dhamana lakini nimepigiwa simu sasa hivi kuwa hawataletwa tena mahakamani kwa kuwa muda wa Mahakama umekwisha na taarifa nilizopokea tumeambiwa wataletwa kesho,”amesema Ngalawa.
Wakizungumza baada ya kauli ya katibu kuwa viongozi hawataletwa mahakamani baadhi ya wafuasi Ikorongo Otto na Masanja Malembeka wamesema kwa sasa hofu imetanda kwa wananchi kwa kuwa huo haukuwa utamaduni uliozoeleka wa kuona viongozi wanakamatwa wakiwa wanadai mali zao.
Awali akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wote wanaoshikiliwa bado wako ndani na watafikishwa mahakamanil leo hata kama muda wa mahakama utakuwa umekwisha watamuomba hakimu.
Amesema dhamana za watuhumiwa ziko wazi kwa kua ni haki ya mtuhumiwa lakini akasema dhamana hiyo inategemea na mazingira ya tukio.
Kamanda amesema bado zoezi la kuwakamata madiwani waliokimbia linaendelea na kuwakata wasiwe wakimbizi badala yake warudi kwenye familia zao kwa kuwa kosa la jinai halina mwisho na lazima watakamatwa kwa uvunjifu wa sheria.
Monday, 18 September 2017
Home
Unlabelled
Msukuma akwama Polisi, mamia wamiminika mahakamani kumsubiri
Msukuma akwama Polisi, mamia wamiminika mahakamani kumsubiri
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment