Jonas Mkude afichua siri ya kusugua benchi - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 6 September 2017

Jonas Mkude afichua siri ya kusugua benchi

Wakati baadhi ya wadau wa soka nchini wakiwa na maswali mengi kutokana na benchi la ufundi la klabu ya Simba nchini ya kocha wao mkuu, Joseph Omog, kumsugulisha benchi nahodha wao wa zamani, Jonas Mkude.Kiungo huyo ameibuka na kufichua siri zito.

Si jambo la kawaida kwa klabu ya Simba kumweka benchi Mkude akiwa sio majeruhi hasa kwenye mechi ngumu, jambo hilo lilitokea hivi karibuni kwenye mechi yanngao ya jamii kati ya Simba na Yanga  na hata hule wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu shooting.

Akizungumzia hali hiyo Mkude amesema hata wakati yeye akiwa katika kikosi cha kwanza kuna wengine walikuwa wakisubiri benchi, hivyo hali hiyo ndio inayomtokea kwa sasa, lakini akaahidi atapambana kurejesha heshima yake.

"Ni kawaida tu,hata mimi nilipokuwa napewa nafasi, kuna wengine walikuwa wanakaa benchi kama mimi kwa sasa, sioni kama kuna ajabu sana kwenye jambo hilo.
" Kinachotakiwa kwa sasa ni kujituma kwa kufanya mazoezi ya nguvu na wenzangu na mengine ya ziada, ili kuweza kumshawishi kocha aweze kuniamini tena na kunipa namba", alisema Mkude.

Alisema kikosi chao kwa sasa ni kipana kina wachezaji wengi waziri hivyo ni lazima mtu ajitume ili aweze kupata namba, tofauti na msimu uliopita.

Kukalishwa benchi kwa Mkude kumeibua maswali mengi hasa kwa mashabiki wa klabu ya Simba, wakimlaum kocha wao Joseph Omog kwamba anataka kuaribu kiwango cha kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment

Popular