Godbless Lema kuanika ushahidi wote wa madiwani waliojiuzulu - KULUNZI FIKRA

Saturday, 30 September 2017

Godbless Lema kuanika ushahidi wote wa madiwani waliojiuzulu

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kesho Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.

Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.

Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.

Lema akizungumza na kulunzifikra blog leo Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

No comments:

Post a Comment

Popular