Leo uongozi wa CHADEMA umekutana na waandishi wa habari kuelezea tukio la kushambuliwa kwa mwanasheria wake Mhe Tundu Lissu na yanayoendelea kuhusiana na tukio hilo.
Katibu mkuu(Mashinji): Lissu alipigwa na bunduki ya kivita na leo ni siku ya tano. Mpaka sasa Lissu ameshafanyiwa operesheni tatu na amechiwa muda wa kupumua kidogo. Kwa wale ambao wangedhani tungefanya hivi vitu haraka haraka, tukatoa michango haraka haraka naomba tujiandae haswa kama chama.
Niwashukuru marafiki zetu wa nje ambao wamelaani tukio hili(Awataja) ikiwemo chama cha wanasheria Kenya, ubalozi wa Marekani na wengineo.
Mpaka jana asubuhi, Tundu Lissu alikuwa ameanza kupata matatizo ya kifua, mguu wake wa kulia umevunjwa vunjwa mara nyingi, mkono wa kushoto, nyonga na mkono wa kulia vimevunjwa vunjwa kwa risasi. Kabla hujafa hujaumbika.
Ameongezewa chupa nyingi sana za damu Dodoma na anaendelea kuongezewa, tulipotoa wito wa kuchangia damu watu walituona sio wa maana lakini wapo watu wengi wanakufa kwa ukosefu wa damu, inatia hasira sana.
Tutaionyesha hasira yetu pale wakati utapofika, pale vyombo vya dola vitapotuletea hao watumiwa wachukuliwe hatua stahiki.
Labda ndio maana wenzetu walisema tumuache hapa lakini kweli hospitali aliopo ina gharama kubwa sana, ni gharama kubwa sana kutibiwa katika hospitali ya Nairobi.
Ujasiri wa Tundu Lissu umejihidhirisha kwa yeye kupigania maisha yake na tunategemea atashinda, tuna safari ndefu sana kuhakikisha Tundu Lissu anapona. Awamu inayofata ni kuunganisha mifupa yake. Kimsingi sisi kama chama tutaendelea kupambana na kutumia resouces kama chama.
Mengine sisi kama chama tunajiandaa kisaikolojia, Tundu Lissu akirudi sio yule Tundu Lissu kwa maumbile yake, tutayapokea kwa sababu ni zawadi ambayo tutakuwa tumepewa na mwenyezi Mungu lakini nina imani Tundu Lissu aliwatatetea watanzania kwa kutumia kinywa chake na unongo wake na ataendelea na yuko imara.
Tulitoa namba ya Esther Matiko na mpaka jana alikuwa amekusanya milioni 11.4 na kwenye akauti ya chama mpaka asubuhi hii tulikuwa tumepata jumla ya milioni 8. Tunashukuru sana, muendelee kutoa kwa moyo huo huo.
Prof. Safari: CHADEMA na wanachama wake na wanaopenda haki hatuna imani na Jeshi la Polisi. Kwa sababu ambazo amezitoa Benson kwa ufasaha, hatuwezi kuliachia Jeshi hili liwatafute watu ambao walitaka kumuua ndugu yetu Lissu.
Kwa hio tunafanya nini? Sisi CHADEMA na tunaopenda haki wote, tunaitaka na tunaidai serikali ilete wapelelezi huru kutoka nje kuja kupeleleza wale ambao walitaka kumuua ndugu yetu Lissu.
Msingi wa kufanya hivi unatokana na kanuni kubwa, tunasema kanuni adhimu ya kimataifa na haki za kibinadamu, haki sio tu itendeke bali ionekane imetendeka na misingi yake hii ipo katika sheria za kimataifa.
Hii ni kigezo cha kujua kwamba haki haikutendeka, kigezo ni mtu wa kawaida akiulizwa nani alitaka kumuua Lissu, jibu atakuwa nini atalisema. Akiulizwa una imani na polisi, hakika atakwambia hana imani na polisi.
Sheria ya ushahidi inazungumza dhana zinazoruhusiwa na mahakama na mtu yeyote yule. Kwamba kama kuna matukio fulani yametokea, kuna dhana gani unazipata, kuna dhana chanya na dhana hasi.
Dhani nini, dhana ni hasi kwamba polisi na serikali vinahusika kutaka kumuua Lissu. Kwa hio, sisi tunaitaka serikali ikubali wapelelezi wa nje waje kuwasaidia. Benson ameelezea kwa ufasaha sana kwa nini Lissu hakwenda kuripoti polisi, polisi wamewakamata mpaka watu waliochangisha michango ya kumtibu Lissu pale Singida.
Lakini mimi namshangaa sana IGP, kama kweli yeye ni IGP, kwanini haijui sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai! Sheria hii kifungu cha kumi kinaelezea namna polisi wanatakiwa kufanya kazi zao, kwamba polisi anafanya upelezi kwenye mazingira gani?.
Moja mtu unaenda kutoa taarifa lakini zaidi ya asilimia tisini hawendi kutoa taarifa, polisi wenyewe wanakwenda kwa sababu ni walinzi wa amani.
Tuesday, 12 September 2017
Home
Unlabelled
Chadema yasema haina Imani na polisi na serikali kuhusu sakata la Tundu Lissu yataka wapelelezi huru kutoka nje
Chadema yasema haina Imani na polisi na serikali kuhusu sakata la Tundu Lissu yataka wapelelezi huru kutoka nje
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment