Bocco aomba kupewa muda zaidi ndani ya klabu ya Simba - KULUNZI FIKRA

Monday, 18 September 2017

Bocco aomba kupewa muda zaidi ndani ya klabu ya Simba

Mshambuliaji wa Simba SC John Raphael Bocco amewaomba mashabiki wa Simba kumvumilia kwa muda kabla ya kuonyesha makeke yake aliyokuwa nayo katika Klabu yake ya zamani ya Azam FC.

Bocco aliyeifungia Simba bao lake la kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga hapo jana amesema anahitaji muda zaidi kwa ajili ya kuonyesha makali yake aliyokuwa nayo hapo awali.

“Kwanza kwa wale ambao wanasema nimeshuka kiwango pole yao kwa sababu bado nina uwezo mkubwa, lakini nahitaji muda zaidi hapa Simba kabla ya kuonyesha makali yangu ambayo nilikuwa nayo Azam FC". Alisema John Bocco

Mchezaji huo wa Zamani Wa Azam FC amesema anaamini akipewa nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ataweza kufunga mabao mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Popular