Arusha: Mtoto mchanga aokotwa kwenye mfereji wa maji machafu akiwa amefariki - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Arusha: Mtoto mchanga aokotwa kwenye mfereji wa maji machafu akiwa amefariki

 Mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 1, ameokotwa katika mtaro wa maji machafu huko Unga Limited

Mwili wa kichanga waokotwa ukiwa umetupwa kwenye mfereji wa maji machafu jijini Arusha

Kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku moja kimeokotwa kikiwa kimefariki na kutelekezwa kwenye mfereji wa kupitisha maji machafu katika eneo la mtaa wa Ali Nyanya kata ya Ungalimited jijini Arusha.

Kulunzifikra blog imefika eneo la tukio hilo ambalo wakazi wake wengi wanajishughulisha na biashara ndogondogo na hapa baadhi ya mashuhuda wanaelezea mazingira ya kichanga hicho kupatikana huku wakilaani kitendo hicho.

Omari Shehe ni mwenyekiti wa mtaa huo ambaye anakemea vitendo hivyo na kuahidi kusaidia vyombo vya dola kumtafuta mhusika ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu kama hiyo.

Vitendo vya utelekezaji na utupaji wa watoto vimeendelea kuota mizizi katika maeneo mengi hususani ya mjini sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kile kinachodhaniwa ni baadhi ya wanaume kukataa majukumu lakini pia kupungua kwa maadili ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Popular