Uvccm waondokewa na mjumbe wa Baraza kuu - KULUNZI FIKRA

Thursday 24 August 2017

Uvccm waondokewa na mjumbe wa Baraza kuu

Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ( UVCCM) kwa mshituko,fezea na huzuni kubwa kwa kupokea taarifa ya kifo cha mwanachama wake na mjumbe wa Baraza kuu Uvccm,Coleman Vincent Massawe kilichotokea usiku wa kuamkia leo.
Katibu wa Hamasa na chipukizi, Joketi.U.Mwengero amesema kifo hicho si tu kimeacha pengo lisilozibika ndani ya jumuiya lakini UVCCM imempoteza kijana wake hodari na mwanachama mwaminifu wa CCM.
Joketi amesema Coleman alikuwa mwanachama shupavu na mpigania Haki za vijana, mtu aliyependa mshikamano na kila wakati alikuwa hachoki kutoa ushauri katika masuala ya msingi kuhusu maendeleo na mstakabali wa jumuiya na ustawi wake.
"Tumeondokewa na mwanachama mwaadilifu na jasiri aliyekipenda chama cha mapinduzi kisera na kiitikadi,pengo lake alitazibika haraka, ametutoka ghafla hazina tulioiandaa katika siku nyingi".
Amemtaja Coloman kuwa amewahi kuwa katibu wa Idara ya hamasa na chipukizi makao makuu ya UVCCM toka mwaka 2015 mpaka 2016, alikuwa mtu mwepesi na mtulivu katika utekelezaji wa majukumu ya jumuiya pia hakuwahi kuyumba au kushiriki usaliti.
"Tumesikitishwa na kifo cha mwenzetu kazi ya Mungu haina makosa,tunatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki, tunamuomba mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na ustahamilivu wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba na maombolezi", amesema Joketi.
Coleman  Vincent Massawe alizaliwa jijini Dar es salaam julai 29 mwaka 1986,aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza kuu mwaka 2013 katika nafasi za uteuzi za mwenyekiti, aliwahi kugombea ubunge jimbo la kawe 2015 na kushiriki shughuli mbalimbali za chama na jumuiya zake.Atazikwa kijijini kwao kibosho sangati mkoani Kilimanjaro jumamosi hii Agosti 26 mwaka huu.
Joketi ametoa wito na kuwahimiza vijana na wanaccm kwa ujumla mkoa wa Dar es salaam na mikoa jirani kujitokeza na kushiriki shughuli za maandalizihadi kumfikisha katika nyumba yake ya milele, marehemu Coleman Vincent.

No comments:

Post a Comment

Popular