RC Dodoma avunja mabaraza ya biashara kwa sababu za kisiasa - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 15 August 2017

RC Dodoma avunja mabaraza ya biashara kwa sababu za kisiasa

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amevunja mabaraza ya biashara mkoani Dodoma kutokana na changamoto mbalimbali ukiwa ni pamoja na kutumika kisiasa.
Akizungumza leo jumanne ofisini kwake, Rugimbana amesema mabaraza yaliyovunjwa ni ya wilaya na la mkoa.
Amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia uundwaji wa mabaraza hayo ndani ya siku saba.
 Amesema mabaraza yatakayoundwa yalenge kutatua changamoto zilizokuwa zikiyakabili.
Pia amesema mabaraza hayo anataka yasimamie uanzishwaji wa viwanda

No comments:

Post a Comment

Popular