Mwenyekiti wa CCM mkoa wa kigoma, Dkt Amani Kaborou amesema ndani ya chama hicho kuna watu ambao hawajakubali mfumo mpya wa uchaguzi unaozuia vitendo vya kupanga safu na hivyo kuibua malalamiko katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza katika mahojiano maalum ofisini kwake kigoma wiki iliyopita ,Dkt Kaborou alisema matatizo mengi wanayo kumbana nayo katika uchaguzi yanatokana na hali hiyo.
Akifafanua maana ya kupanga safu, alisema ni vitendo vya baadhi ya viongozi kutoa fomu kwa watu wanaowataka wagombee au kuwanunulia kadi za uanachama watu wengi ili baadaye waweze kuwachagua.
Alisema katika utaratibu huo,baadhi ya viongozi huficha fomu na kuwapa wagombea wao.
"Matatizo tunayokubana nayo katika uchaguzi yanaweza kusemekana yanaanzia na uchaguzi huu, kwa kuwa umekataza kanisa kupanga safu,yaani kuteua watu ambao baadae watakuja kukupigia kura wewe katika awamu yako", alisema.
Alisema kuna mahali ambako watu au viongozi wa kata hawakuwa tayari kuhafiki utaratibu mpya wa chama na pale walipojaribu kuendeleza wanachama waliwasilisha malalamiko yao ngazi za wilaya hadi mkoa.
" Hilo la safu kwa kweli naona watu wengi wanasema mini! Naona hilo limekuwa kila mahali tangu ngazi ya tawi na kata ",alisema Kaborou aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chadema na mbunge kupitia chama hicho.
Alikataa kuingia kwa undani kwa kuwa vikao havijayajadili ,Dkt Kaborou alisema "Wanachama wanasema kanisa 'tulikuwa tunapangwa na viongozi' na wanashangaa utaratibu wa uchaguzi safari hii kwamba mtu anajichukulia fomu mwenyewe"
Saturday, 12 August 2017
Home
Unlabelled
Mfumo wa uchaguzi wa ndani ya CCM bado kizungumkuti
Mfumo wa uchaguzi wa ndani ya CCM bado kizungumkuti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment