Bukoba. Manispaa ya Bukoba imeendelea kuwa katika headline baada ya uchaguzi uliofanyika mapema leo hii Kufuatia uchaguzi huo wa kumpata naibu meya uliofanyika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ukihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo mh Wilfred Lwakatare na meya wa manispaa hiyo Chief Kalumna umefanyika kwa uangalizi mkubwa ambapo viongozi wote wameendelea kubaki katika nafasi zao akiwemo Naibu meya Jimmy Kalugendo ambaye pia ni diwani wa kata Nshambya na kufanya manispaa hiyo kuendelea kuongozwa na CHADEMA kwa nafasi zote za juu.
Uchaguzi huo wa kumpata Naibu meya na viongozi wa kamati umefanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu Za balaza ambapo Kila baada ya mwaka waga unafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi hizo Baada ya uchaguzi huo.
Mbunge Lwakatare amewapongeza wajumbe wote walioshiriki katika uchaguzi huo kwa kufanya uchaguzi wa Amani hali iliyopelekea viongozi wao kuendelea kushikilia nyadhifa hizo. Aidha Lwakatare amewaomba madiwani na watendaji wa manispaa hiyo kundelea kushirikiana kwa Karibu sana katika suala zima la kuwaletea maendeleo.

No comments:
Post a Comment