Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu imetaka upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili Rais wa klabu ya simba Evas Aveva na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama kaburu kuelezea upelelezi umefikia wapi?
Hakimu mkazi mkuu,Victoria Nangwa alielezea hayo baada ya mwendesha mashtaka mwandamizi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ,Leonard Swai kudai upelelezi bado ujakamilika .
Swai aliomba apewe siku 14 kwa ajili ya kukamilisha ripoti ya polisi ya upelelezi ambayo wanaisubiri .
Kwa upande wa wakili wa utetezi,Mutakyamirwa Philemon aliomba mahakama itoe siku saba, lakini Swai alisisitiza kuomba siku 14 kama ilivyo kwenye kesi nyingine.
Kesi hiyo imeairishwa hadi Agosti 30 2017,kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutakatisha fedha za kigeni dola 300,000 za marekani.

No comments:
Post a Comment