Katibu wa soko la sido ashikiliwa kwa uchochezi - KULUNZI FIKRA

Sunday, 20 August 2017

Katibu wa soko la sido ashikiliwa kwa uchochezi

Wakati hali ya amani na utulivu ikiwa imerejea katikati ya jiji la Mbeya baada ya kutokea vurugu juzi mchana, jeshi la polisi limesema linawashikilia watu 18 akiwemo katibu wa wafanyabiashara wa soko la sido, Alanus Ngogo kwa tuhuma za kuchochea vurugu hizolile Juzi mchana, polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na upupu kuwatawanya wafanyabiashara wa soko hilo waliokuwa wamegoma kuwekeza agizo la serikali kuwataka kutoendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu ndani ya soko hilo ambalo liliteketea kwa moto na kuunguza mali zote usiku wa kuamkia Agosti 15.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,Mohammed Mpinga alisema kwamba baada ya kutokea kwa vurugu kuna watu waliokuwa  katika soko hilo la sido waliingia na kufunga barabara kuu ya Tanzania-Zambia kwa mawe na magogo huku wakipiga mawe magari yaliyokuwa yakipita.
"Katika tukio la juzi tuliwakamata watu 18 hwa kwa kosa lao ni kuingia barabarani na kuanzia kupaga mawe na magogo na kuzuia magari yasipite barabara kuu ya Tanzania-Zambia kuanzia kabwe mpaka mafiati.
"Lakini yule katibu wa soko (Alanus Ngogo) yeye anatumiwa kwa kosa la uchochezi kwani juzi ile mimi nilipopanda jukwaani na kuwataka watu wote waende nyumbani kwao kwa usalama wao yeye alichukua kipaza sauti na kuanzia kuamasisha watu wasiondoke eneo lile akitamka 'tutakesha hapa hapa' na maneno mengine ya kukashifu", alisema kamanda Mpinga.
Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya kumaliNtinika  kwa  mahojiano  watapandishwa kizimbani kujibu tuhuma zao.
Kuhusu hali ya usalama,kamanda Mpinga alisema ulinzi katika jiji hilo umeimarishwa na polisi wapi doria muda wote na watu waliamkaa alfajiri kuendelea na shughuli zao maeneo mengi hususani Soweto,kabwe, mwanjerwa hadi mafiati ambalo juzi biashara zilifungwa kutokana na usalama kuwa mdogo .
Hata hivyo, serikali ya mkoa wa Mbeya kupitia kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika ilisisitiza kusimamia msimamo wake wa kutowaruhusu wafanyabiashara hao kuendelea na ujenzi wa vibanda vya tofauti na ombi lao kutaka kuruhusiwa.
Ntinika aliwataka wafanyabiashara hao kuwa na hali ya utulivu na uvumilivu kwa kusubiri siku tano zilizotengwa na serikali ili kupisha kamati maalum iliyoundwa kufanya tathmini ya hasara iliyojitokeza kutokana na janga hilo pamoja na kuchunguza kiini cha moto huo.

No comments:

Post a Comment

Popular