Msanii Fareed Kubanda ambaye wengi humuita 'concious rapper' kutoka bongo, amejibu kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe aliyosema wasanii wasiimbe siasa, na kusema kuwa siyo rahisi kwa wasanii kuacha kitu kitu hicho.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Fid Q amesema Waziri hakuwa sahihi kusema hivyo, kwani siasa ipo kwenye maisha yetu ya kila siku, ambayo wasanii ndiyo kitu ambacho hutazama ili kuweza kufanya kazi zao.
"Nafikiri suala la Waziri wa Habari kusema wasanii wasiimbe siasa halikuwa sahihi, nafikiri labda alitaka asema wasanii wasiwaimbe wanasiasa, kwa sababu siasa ni sehemu ya maisha yetu, na tunaguswa nayo kwa namna moja au nyingine, tunataka au hatutaki, na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka ili mradi hujavuka mstari, na kazi ya msanii ni kuelimisha jamii si tu kuburudisha", alisema Fid Q.
Fid Q aliendelea kusema kuwa hata mafanikio ambayo Mh. Waziri aliyazungumzia, anatakiwa atambue kuwa msanii kufanikiwa sio kuwa na mali tu, hata kubadilisha jamii kupitia sanaa yake ni mafanikio makubwa.
"Bob Marley aliimba siasa mpaka leo tunatambua legacy yake inaendelea kuishi, Fela Kuti pia, alafu mafanikio ya msanii siyo lazima masuala ya pesa, magari sijui majumba, mafanikio kwa msanii ni namna sanaa yake inaweza kubadilisha jamii, na kuamini kwamba pesa, magari na nyumba za kifahari ndiyo vitu vya mafanikio, si nadharia nzuri na yenye busara kwenye jamii", alisema Fid Q.
Monday, 14 August 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment