Chadema yaibua mapya kuhusu 'bombardier' - KULUNZI FIKRA

Friday, 18 August 2017

Chadema yaibua mapya kuhusu 'bombardier'

 
CHADEMA kupitia kwa mwanasheria wake mkuu, Tundu Lissu, imeishauri serikali kuwa makini katika kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu ubadilishaji na uvunjaji wa mikataba ya uwekezaji ikiwemo ile ya madini, ili kuiepusha nchi kuingia katika hasara endapo wawekezaji hao wataishtaki mahakamani.

Katika mkutano wake na wanahabari, Lissu amedai kuwa chama hicho kimepata taarifa kuwa, kampuni mbili za madini ambazo ni Acacia pamoja na Anglo-Gold Ashanti, zimetoa notisi ya kuishtaki serikali kufuatia uamuzi wake wa hivi karibuni wa kuzuia usafirishwaji wa mchanga wenye madini, huku akibainisha kuwa endapo serikali itashindwa kwenye kesi hizo, italazimika kulipa fidia zaidi ya dola za Marekani bilioni Mbili.

KUHUSU BOMBADIER

Tundu Lissu pia amehoji sababu za ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier hakutofika  kama ilivyoahidiwa licha ya Serikali kuahidi kuwa ingefika mwezi Julai, mwaka huu.

Amesema kwa taarifa walizonazo ni kwamba ndege hiyo imekamatwa na kushikiliwa nchini Canada na wadeni wa Tanzania kutokana na kuvunjwa kwa mkataba uliokuwepo.

Mwanasheria huyo wa CHADEMA amedai kwamba Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Augustine Mahiga alikwenda nchini Canada na kuwataka wahusika kuficha siri.

Hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa twitter Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa baada ya kuhojiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuhusu ilipo ndege hiyo, alijibu kuwa ndege hiyo itawasili na kwamba kuna taratibu za mwisho zinafanywa kabla ya kuwasili kwake.

No comments:

Post a Comment

Popular