Sakata la kumng'oa meya wa jiji la Mwanza ,James Bwire , limechukua sura mpya mpya baada ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ( ccm) mkoa wa Mwanza kuwahoji viongozi wa serikali.
Taarifa zilizotufikia kutoka kwa baadhi ya viongozi wa ccm mkoa wa Mwanza,zinadai kwamba kamati ya siasa ya mkoa juzi iliwahoji mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mary Tesha na mbunge wa Nyamagana Stanislaus Mabula.
Wengine waliohojiwa ni meya Bwire, Naibu Bhiku katecha, katibu wa wa ccm wilaya ya Nyamagana, Diwana wa kata ya mkoloni ,Dismas Rite, Danatha Gapi( mkuyuni), John Minja (Igogo),Musa Magabe (Igoma) na Vicent Tegge wa Lichelele.
Hatua hiyo imefikiwa baada vikao viwili tofauti ndani ya siku mbili kutokana na madiwani 19 kati ya 21 kutia saini ya mashtaka 23 dhidi ya ya meya Bwire. Katibu wa Itikadi na uenezi wa ccm mkoa wa Mwanza, Simon Mangelepa, amethibitisha kuhojiwa kwa viongozi hao ingawa ingawa hakufafanua zaidi.
"Ni kweli kamati ya siasa ya mkoa imekutana leo ( juzi) kujadili mgogoro wa Meya,Mkurugenzi na madiwani.Kuna baadhi yao watahojiwa, siwezi kuwaambia kwa sasa kwa sababu ni mimi sijui ni nani na nani wapi kwenye orodha ya kuhojiwa, ila wakikamilisha na kunielekeza kutoa taarifa yake tutafahamishana", Alisema.
Aidha Mangelepa hakuwa tayari kuelezea uwepo wa kamati ya maadili na usalama ya ccm ngazi ya taifa ambayo inadaiwa kufika Mwanza kushughulikia migogoro huo,bali alisema anachokitambua ni kuwatoa baada ya ya kamati ya ya siasa mkoa kumaliza,ingebainisha mgogoro huo ushughulikiwe kwa ngazi gani.
Kulunzifikra blog ilishuhudia juzi viongozi wakiingia kwa zamu katika ofisini kwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza Anthony Diallo kuhojiwa.
Aliyekuwa wa kwanza kuingia ofisini humo ni mkuu wa wilaya ya Nyamagana na Naibu meya.
MGOGORO ULIVYOANZA KUIBUKA
Mgogoro huo uliibuka katika kikao cha madiwani Agosti 15, mwaka huu baada ya diwani wa makuyuni, Donatha Gapi ambaye ni katibu wa madiwani wa ccm kusimama na kuwasilisha hoja hoja ya kutaka mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni meya asiwe na mwenyekiti badala yake kiti kikaliwe na Naibu wake.
Hoja ya Gapi iliwasilishwa kabla ya meya Bwire kusimama kufungua kikao hicho kitendo ambacho kilidhirisha kuwepo mkakati wa kumng'oa .
Hata hivyo meya Bwire alifanikiwa kupangua hoja ya diwani huyo na kufungua kikao hicho ,huku akiwaonya wajumbe kutojadili yeye kwa vile haikuwa moja ya ajenda zilizopo mezani kwake.
Kutokana na majibu hayo,Mbunge Mabula aliingilia kati na kumshauri meya kuondoka ili Naibu meya wake aendeshe kikao,lakini ushauri huo haukuweza kufua dafu.
Baada ya Mabula kuketi Meya Bwire alisimama kwa Mara nyingine kusisitiza kuwa hawezi kuondoka,hivyo akawataka madiwani kujadili kilichowasilishwa mezani hatua ambayo iliwafanya kutokana nje ya ukumbi kumwacha yeye ni madiwani watatu wanaomuunga mkono.
Sunday, 20 August 2017
Home
Unlabelled
CCM yatia mguu mgogoro wa Meya Mwanza
CCM yatia mguu mgogoro wa Meya Mwanza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment