Nyumba ya Anna Mkapa, Mke wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa imekumbwa na bomoabomoa inayoendelea pembeni mwa Barabara ya Morogoro baada ya kuwekewa alama ya “X.”
Nyumba hiyo ipo katika shamba linalomilikiwa na familia ya Mkapa lililopo eneo la Mbezi kwa Msuguri, maarufu kwa jina la Kituo cha Zamani na ubomoaji huo unafanyika ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayounganisha Dar es Salaam na mikoa mingine.
Nyumba hiyo iliyozungushiwa ukuta na yenye duka imekutwa na tashtiti hiyo baada ya watu waliokutwa katika nyumba hiyo kuthibitisha kuwa nyumba hiyo ni ya Mama Anna Mkapa na kugoma kuzungumza chochote mpaka wawasiliane na mmiliki huyo.
“Ni kweli hapa ndiyo nyumbani kwa mama Anna Mkapa, lakini mimi siwezi kuzungumza chochote kwa sababu si mhusika. Hapa ni kama mwangalizi wa nyumba tu. Naomba mtafute mama (Anna Mkapa) mwenyewe. Nendeni ofisini kwake. Mimi hapa ameniachia tu kama mwangalizi wa nyumba yake, kwa hilo mtanisamehe siwezi kuzungumza,” alisema .
ndugu wa mke wa Rais wa awamu ya tatu ambaye alikuwa akiuza duka lililoko nje ya nyumba hiyo, iliyowekwa alama x.
Hata hivyo mwangalizi wa nyumba hiyo alimtaja jirani yao mmoja ambaye ni Babu kipofu kuwa yeye ndiye anayefahamu mengi kuhusiana na historia ya eneo hilo.
James Shirinde mwenye mika 80 ndiye jirani mwenyewe ambaye alikiri kufahamu vizuri historia ya eneo hilo na kueleza jinsi alivyonunua eneo hilo ambalo kwa sasa linamilikiwa na familia ya Mkapa.
“Nilinunua eneo hilo mwaka 1975 wakati huo nikiwa mfanyakazi wa Shirika la Reli ambalo kwa wakati huo lilijulikana kama TRC na huku kulikuwa ni mashamba tu,” alisema.
“Mwaka 1980, mke wa rais mstaafu alikuja akanunua shamba na akajenga nyumba ambayo mpaka sasa anaishi mdogo wake, Rose Silayo.”
“Haya mawe waliyoyaweka sasa yametukuta baada ya kutungwa sheria mpya ya Hifadhi ya Barabara ya mita 121.5 mwaka 2007 na 2009. Wakati huo mke wa Mkapa naye alikuwa amejenga nyumba yake na mumewe pia alikuwa amenunua shamba huku la ekari tano,” alisema.
Mhandisi wa TANROADS, Johnson Letechura alipoulizwa kuhusu alama ya bomoa katika nyumba hiyo, alijibu kwamba nyumba yoyote ambayo ipo katika hifadhi ya barabara itabomolewa

No comments:
Post a Comment