Bodaboda waanzishiwa kipindi kwenye televisheni - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 15 August 2017

Bodaboda waanzishiwa kipindi kwenye televisheni



Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Usalama barabarani, Teopista Malya amezindua kipindi cha bodaboda kitakachokuwa kinarushwa kwenye televisheni ya Clouds.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Agosti 15 amesema kuwa kipindi hicho kiwahusishe wataalamu mbalimbali kutoka wakala wa usafiri wa Nchi kavu na Majini(Sumatra) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wawaeleweshe madereva pamoja na watumiaji wa usafiri huo.

Amesema kuwa Serikali inawathamini waendesha bodaboda na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwataka kutii sheria zilizowekwa ili kupunguza ajali ambazo nyingi zimesababisha vifo na ulemavu wa kudumu.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka amesema kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.

Pia, ametumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.

Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos amesema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo

No comments:

Post a Comment

Popular