Bodaboda marufuku kupakia watoto mwenye umri wa nchini ya miaka tisa - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 15 August 2017

Bodaboda marufuku kupakia watoto mwenye umri wa nchini ya miaka tisa

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limepiga marufuku madereva pikipiki maarufu bodaboda kuwapakia watoto wenye umri chini ya miaka tisa

Dereva yeyote atakayekiuka agizo hilo atakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani ambapo anaweza kuhukumiwa kwenda jela au kulipa faini kulingana na hakimu atakanyoamua

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kipindi cha 'Bodaboda' ambacho kitaonyeshwa kwenye televisheni ya Clouds, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ACP Theopista Malya, alisema kuna tabia ya madereva wa pikipiki kukodishwa kuwapeleka watoto wadogo shule jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"katika mambo ambayo sheria za usalama barabarani zinazomwongoza dereva wa bodaboda mojawapo ni kupakia watoto wenye umri chini ya miaka tisa. Unakuta anabeba watoto wanne kwenye pikipiki moja na mwingine mdogo yupo mbele yake.

"Licha ya kwamba ni kosa kisheria lakini pia ina athari kubwa sana kwa usalama wa mtoto mdogo kwani upepo unampiga kwa kasi hivyo hawezi kustahimili hali hiyo mwishowe anapata magonjwa", alisema ACP Malya.

Kuhusu elimu kwa madereva hao, bosi huyo wa kikosi cha usalama barabarani alisema polisi kwa kushirikiana na kamati ya usalama barabarani nchini wameweka mikakati ya kupunguza ajali ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha utoaji elimu kwa waendesha bodaboda.

No comments:

Post a Comment

Popular