Apanda kizimbani kwa kujifanya msemaji wa Ikulu - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 15 August 2017

Apanda kizimbani kwa kujifanya msemaji wa Ikulu

Mfanyabiashara Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu akikabiliwa na shataka la kujitambulisha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa habari wa Ikulu , Gerson Msingwa.
Akisoma hati ya mashtaka Jana wakili wa serikali, Jacquline Nyantari alidai kuwa kati ya ya juni 28 na julai 4 2017 Dar es salaam  kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa habari wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi .
Amedai kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia  ya udanganyifu.
Mshtakiwa alikana shtaka upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado  ujakamilika,mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 1 milioni,kesi imeairishwa mpka Agosti 23 2017 mwaka huu.Mtuhumiwa akuweza kukamilisha masharta ya dhamana na kurudishwa rumande

No comments:

Post a Comment

Popular